BORESHA YOUTUBE CHANNEL YAKO KWA HIZI APP.







 Utangulizi

Kama wew ni "youtuber" bilashaka umekua ukiuumiza kichwa jinsi ya kupata viewers wengi na subscriber wengi.Hivyo unaweza ukapata viewers /watazamaji wengi kwa njia ya kuunda video bora zenye ubunifu mkubwa,na pia kuweka picha ya kuvutia juu yake,Hayo yote utaweza kuyafanya kama utakua unatumia Application sahihi na yenye uwezo.Leo nimekuletea App bora ambazo watu wanazitumia katika kuedit video zao na kuedit picha hata kwakutumia simu yako.


Zifuatazo ni  Application ambazo hutumika kutengenezea na kufanyia editing video za youtube.










KINEMASTER

Hii ni App ambayo hupatikana kwenye simu za android na ios,pia hupatikana hata kwenye windows/computer.Hii App hutumika kufanya editing za video ,yani editing yeyote ile unayoijua unaweza kuifanya kwakutumia hii App,tools zipo nyingi sana ambazo unaweza kuzitumia kuifanya video yako kuwa vile unavyotaka wew,mfano:Unaweza kubadilisha background ,kuwekea sauti mpya,kuwekea maandishi,kuweka maandishi yanayotembea,kuunganisha vipande mbalimbali vya video,kuweka rangi uzipendazo,kutengenezea slide kama za kwenye power point,nk.

Hii App ya kinemaster inapatikana playstore na hata kwa watumiaji wa iphone pia hupatikana ,ila usiidownload playstore kwasababu watataka ulipie ili uweze kutumia kwa kupata tools zote,sasa inatakiwa uidownload google andika "download free kinemaster without water mark".watermark ni nembo yao ambayo itakua inaonekana kwenye video zako chini,sasa ukidownload kinemaster free without water mark hayo maneno hutoyaona.



PICSARTS

Hii ni Application ambayo hutumika kutayarishia youtube thumbnails/picha za juu ya video za youtube,Faida kubwa yakutumia hii App inakuwezesha kuunda picha itakayo fit moja kwa moja youtube,yani kuna sehemu ya kuchagua kama unataka picha yako ukatumie youtube,twiter,facebook,instagram,pintest .Hivyo utachagua youtube kisha picha yako itatoshea moja kwa moja youtube,kwakupitia hii App itakuwezesha kuweza kuunda picha zenye mvuto zaidi ambazo utazitumia kubandika juu ya video zako za youtube.Hii App inakuwezesha kuedit picha katika muundo wowote ule ambao unautaka,Mfano:unaweza kuondoa background za picha yeyote na kuwekea background mpya,unaweza kuandika maneno juu ya picha yako kwa miundo tofauti tofauti kama italic,bold,latin,nk,pia unaweza kuandika maandishi kwa rangi tofautitofauti.





YOUTUBE STUDIO

Hii Application wengine wanaiita yt-studio,Hii kazi yake kubwa ni kumanage youtube channel yako,Hii sasa ndoutumika kuwekea thumbnails zako,unaweza kuweka na kutoa thumbnails zako muda wowote kupitia hii Application,pia unaweza kujibu comment kirahisi kupitia hii Application,Pia hii Application ndo hutumika kuweza kuona statistics zote kuhusu channel yako,mfano unaweza kujua visitors wanaotembelea kwa siku,watching hours zako na taarifa  zako  zote muhimu za channel yako hupatikana kupitia hii App.










Post a Comment

Previous Post Next Post