Utangulizi
Bilashaka umeshawai kusikia kuhusiana na namna ya kufanya kazi online na kulipwa,Zipo kazi nyingi sana ambazo unaweza kuzifanya online na kulipwa pesa kama kawaida.Mfano wa hizi kazi ni kukamilisha survey,kuandika(typing job),kufanya kazi ndogondogo(microtasks) , kazi ambazo ni rahisi kwa binadamu kufanya ila ni ngumu kwa computer( Human intelligents tasks),kujaza captcha,nk.
•Hapa tutaangalia namna ya kutengeneza pesa kwa njia ya kuandika captcha.
Captcha,Ni mfumo ambao hutumika kuweza kutambua kama ni mtu ndiye anayetaka kuingia katika tovuti fulani au App,Hivi huyo mtu ataitajika kuweza kujaza maneno fulani ,kama akipatia kuyajaza ndipo system itafunguka.Hii system imeundwa ili kuweza kuzuia robot au automated system kuweza kuingia kwenye tovuti mbalimbali.
Ebu tuangalie jinsi ya kufanya kazi ya kuandika kwa kutumia 2captcha.
2Captcha,Hii ni website ambayo inawezesha kuandika/kujaza captcha,Kupitia hii tovuti itakupa uwezo wa kuweza kufanya kazi iyo.
•Jinsi ya kujiunga na hii tovuti ya 2captcha.
Ingia google chrome andika 2captcha.com kisha bonyeza walipoandika sign up,Jaza taarifa zako watakazotaka ujaze,bilashaka watataka ujaze email kisha watataka uverify iyo Email kwenye gmail.
Baada ya kujisajiri inatakiwa u log in kwenye 2captcha,baada ya kulog in hapa watakupa test ya maneno 15 kujaza ,unatakiwa ufanye kwa umakini mkubwa sana ili uweze kuepuka kukosea.ukikosea hutolipwa, pia kama ukikosea sana akaunti yako itafungwa.
Je ?Naweza kupata kiasi gani cha pesa kwa kufanya kazi hii,
Jibu, utaweza kupata kuanzia dollar 0.3$ hadi 5$ kwasiku, kwani maneno 1000 ni sawa na 0.3$.Ila wapo watu ambao wanafikisha mpaka 100$ kwa mwezi.
Jinsi ya kuwithdraw pesa kutoka 2captcha.
Zipo njia mbalimbali za kuweza kuwithdraw pesa utakayoipata kwenye 2captcha.Njia hizo ni Bitcoin,Usdt,Bitcoin cash Advcash,webmoney,peferfect money,Airtm na payer.kiwango cha kuweza kuwithdraw utegemeana na njia utakayotumia.




Post a Comment