- Utangulizi.
Bila shaka umeshawahi kusikia/kujifunza kuhusiana na vitamin,Leo nimekuletea makala hii fupi ambayo itaangazia faida za vitamini mwilini na vyanzo vyake.Vitamin ni virutubisho vinavyopatikana kwenye baadhi ya vyakula,mfano makundi kama ya matunda ,mboga ,nafaka,nyama ,pia jua la asubuhi (vitaminiD),nk.
Vyanzo vya vitamin
Tunapata vitamin kupitia vyanzo vikuu,ambavyo ni vyakula,ikiwemo baadhi ya makuni ya vyakula na matunda.
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo hutupatia vitamin:-
•Samaki
•Mayai
•Nyama ya kuku
•Viazi vitamu
•kabichi
•Kitunguu
•Nyanya
•Uyoga
•Maharage
•Alizeti
•Maziwa
•Soya
•Karanga
•Ukwaju
•Numbu
Yafuatayo ni baadhi ya matunda ambayo hutupatia vitamin:-
•Ndizi
•Strawberry
•Apple
•Chungwa
•Limao
•Parachichi
•Papai
•Karoti
•Boga
•Firisi
•Piripiri O
•Tikiti
•Nanasi
•Pera
Umuhimu wa vitamin mwilini.
- Husaidia kuimarisha kinga ya mwili ambayo hupelekea kupambana na magonjwa.Vitamin A huusika.
- Husaidia kuimarisha mifupa na meno.Vitamin D ufyonza calcium ambayo ufanya mifupa na meno kuwa imara.
- Vitamin C husaidia kupona kwa haraka kwa vidonda.
- Vitamin A husaidia kuona vizuri.
- Husaidia ngozi,macho na mifupa ya fahamu kuwa na afya nzuri,makundi ya vitamin B huusika.
- Husaidia mwili kufyonza nguvu kutoka kwenye vyakula tunavyokula mwilini.
- Vitamin K husaidia damu kuganda kwa haraka.
- Vitamin E husaidia kuimarisha umbo la cell kwa kulinda ukuta wa cell.

Post a Comment