UTANGULIZI
Bilashaka umekua ukisikia neno hili forex mara kwa mara,Leo nimekuletea makala hii ya utangulizi kuhusu biashara ya hii ya forex.Ila ili uweze kufanikiwa kwenye biashara hii inatakiwa ujifunze sana,kwani kama hutokua na maarifa yakutosha basi hutoweza kupata faida na utakua mtu wakupata hasara tu,kwaiyo inabidi ujifunze kwanza.
Nitakuletea makala za jinsi ya kufanya hii biashara kwa kutumia mfumo wa automated forex trading.(Robot),huu ni mfumo ambao unajiendesha wenyewe haiitaji ujuzi wowote.(fuatilia makala zijazo ili uweze kujua zaidi)
•Forex ni nini?
Forex ni ubadilishaji wa Fedha za kigeni yaani Foreign Exchange, na neno Forex, ni ufupisho wa maneno hayo yaani Foreign Exchange.
•Je mtu yoyote anaweza kujifunza na kufanikiwa?
Ndio kila MTU mwenye akili timamu anaweza kujifunza na kufanikiwa bila shida yoyote
•Naweza ku-trade Forex muda wowote?
Biashara ya Forex, inawezeshwa na Forex brokers, ambao huwa wanatoa uwezo au access ya kuuza na kununua fedha za kigeni, pindi masoko ya kubadilisha fedha za kigeni yanapofunguliwa, Masoko haya hufanya kazi kwa muda wa kazi wa nchi husika, mara nyingi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni kwa masaa ya nchi husika, nchi hizo ambazo zina masoko ya kubadilisha fedha za kigeni ni Marekani ambayo ina masoko makuu mawili (New York Stock Exchange na NASDAQ), Uingereza ambayo ina soko la London Stock Exchange, Ujerumani, Japan, Australia na New Zealand. Masoko haya hufunguliwa kwa masaa tofauti tofauti kulingana na time zone ya nchi husika na hufungwa nyakati za weekend, yaani Jumamosi na Jumapili.
•Je kwenye forex kuna kuuza bidhaa yoyote au kiingilio?
Jibu pia ni hapana hakuna bidhaa wala pesa ya kiingilio utakayolipa kwa mtu yoyote yule
•Je Forex ni utapeli kama biashara za Upatu?
Jibu jepesi ni HAPANA. Forex trading ni biashara halali kabisa inayoratibiwa na mashirika ya kiserekali kulinda mambo ya kitapeli ya siweze kutokea na imekuwepo kwa miaka mingi na itaendelea kuwepo, na haina uhusiano wala haifanani na biashara za Upatu wala kubet
•Je nahitaji elimu gani ku-trade Forex?
Huhitaji elimu yoyote maalum kuwa mfanya biashara mzuri wa Forex
•Je nahitaji mtaji kiasi gani kuanza Forex?
Mtaji wa kuanza Forex ni elimu ya hii biashara au ujuzi, swala na mtaji wa hela ni wew mwenyew utakavyoamua
•Je faida ya Forex inapatikana vipi?
Faida hupatikana pale utakapo kununua pair katika gharama ya chini na thaman(price) kupanda au kuongezeka na ikishuka ukiwa umenunua utapata hasara, au ukiuza pair katika thamani yajuu na ikaendelea kushuka, hapo utapata faida vile vile ikipanda wakati umeuza utapata hasara...yote haya inabid ujifunze ili kujua sehemu sahihi ya kuuza na kununua
•Je forex inaweza kunitoa kimaisha?
Jibu ni ndio kama utajifunza kwanza namna hii biashara inavyofanyika pia ukazingatia nidhamu ya biashara na bila kukata tamaa itakutoa kimaisha
•Je elimu inapatikana wapi?
Kutokana na hakuna mfumo rasmi wa kufundisha biashara yoyote duniani inakupasa kutafuta mtu mwenye ujuzi na uzoefu na hii biashara ili kupata ujuzi utakao kusaidia kufanikiwa
•Je urahisi wa hii biashara upo wapi?
Hii biashara unaweza kuifanya popote hata kitandan kwako, haihitaji kutafuta mteja wala kuanza kusumbuana na watu
•chamsingi ni ujuzi wa kuifanya hii biashara ndio kunahitajika pekee, ambao UNAHITAJI kujifunza kwa MTU mzoefu.

Post a Comment