Kwa dunia ya leo kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali mtandaoni,kwasababu ya bei yake kuwa ni nafuu sana.Mfano wa vitu ambavyo unaweza kuvinunua online ni Mavazi(nguo za aina zote), vifaa vya umeme kama Computer,simu,Radio,Extension,taa za umeme,majiko ya umeme,majagi ya umeme,vyombo vya ndani,vyombo vya kufanyia kazi,vifaa vya maofisini na viwandani,Magari,pikipiki,baiskeri
Hivyo ili uweze kufanya hayo manunuzi
mtandaoni inatakiwa uwe na application maalumu itakayo kuwezesha kununua izo bidhaa mtandaoni.
Zifuatazo ni baadhi ya Application muhimu ambazo zinatumika kununua vitu mtandaoni .
•Kikuu
Hili ni moja kati ya soko maarufu la mtandaoni ambalo uuza bidhaa mbalimbali.kikuu ilianzishwa mwaka 2015 na mwanzilishi wake akiwa anaitwa Mr.Xu Zheng(CEO), Hii kikuu imelengwa zaidi kutoa huduma kwa nchi za barani africa.Na ni rahisi kuweza kununua bidhaa kupitia App ya kikuu,kwasababu ya njia ambazo unaweza kutumia kufanyia malipo ni zakawaida sana,pia uaminifu wao ni mkubwa na wanamawakala wao ambao ni watanzania wanaosambaza bidhaa,bidhaa ambazo unaweza kununua kupitia hii App ya kikuu ni Nguo za aina zote,Simu za aina zote,Vyombo vya ndani,vifaa vya umeme karibia vyote.
Jinsi ya kufanya ili uweze kununua bidhaa kwenye App ya kikuu.
i.Download App ya kikuu playstore au sehemu yeyote.
ii.Jisajiri kwa majina yako kamili na anuani za mahali unapopatikana au unapoishi(Hakikisha unajaza taarifa zako kamili ili kurahisisha bidhaa iweze kukufikia kiurahisi)
iii.Baada ya kujisajiri kikamilifu,log in kwenye akaunti yako kisha chagua bidhaa unayoitaka (Add to cart) ,kisha fuata utaratibu husika(hapo kuna hatua chache utazifuata ikiwepo kufanya malipo na kujaza taarifa za mahali ulipo na namba za simu ambapo utapokelea mzigo) ,hakuna cha kuhofia kwasababu utakua ukipokea taarifa za mzigo kua upo wapi mpaka kukufikia.
•Amazon
Hii ni kampuni kubwa sana ambayo imeteka soko la dunia kwa uuzaji wa bidhaa mtandaoni,Kampuni hii ya amazoni ilianzishwa mnamo July 5 mwaka 1994 na mwanzilishi wake akiwa anaitwa jeff bezos(Huyu mwaka 2019-2020 alishikilia record ya kua tajiri wa kwanza duniani kwa kumpita bill gett,napo 2021-2022 alinyang'anywa nafasi hio na Elon musk)
Jinsi ya kufanya ili uweze kununua bidhaa kupitia hii app ya Amazon.
i.Download App ya amazon plastore au sehemu yeyote.
ii.Jisajiri kwa majina yako kamili,weka Email inayotumika na namba ya simu sahihi.
iii. Log in kwenye akaunti yako,kisha utachagua bidhaa unayoitaka (Add to cart),kisha utafuata utaratibu utakao ambiwa,kwani ni rahisi tu,itakubidi kulipia kwa kujaza namba zako za card ya bank ili kufanya malipo.Ni vyema pia kuangalia kama utalipia gharama ya kusafirishia(shipping fees) au hapana ,ili ujue mapema.
•Kupatana.
Hii pia ni moja kati ya App maarufu sana Tanzania ambayo inamuwezesha mtu kuweza kuuza na kununua bidhaa mtandaoni.Mfano wa bidhaa ambayo unaweza kununua ni magari,Simu,vitanda,Sofa,simu,Tv,pasi ,Radio ,nk.(Ila vitu vinavyouzwa kupitia hii App ni vilivyotumika na vipya pia vinapatikana).
Jinsi ya kuweza kununua bidhaa kwenye App ya kikuu.
i.Download App yako kwenye playstore.
ii.Jisajiri kwa taarifa zako kamili ,ikiwemo majina yako kamili,anuani zako kamili na namba zako sahihi za simu.
iii. Log in kwenye App yako,kisha chagua bidhaa yako unayotaka kununua ,kisha fanya mawasiliano na muuzaji.
Pia hata kama ukitaka kuuza bidhaa yako kwenye hii app ya kupatana itakubidi uweke tangazo la kuuza bidhaa yako,Hapa utafuata utaratibu uliopo ndani ya App yako.
•Beforward.
Hii ni kampuni namba moja japani inayoongozo kuuza magari yaliyotumia sehemu mbalimbali duniani.Hii kampuni inauza magari pamoja na vipuri vyake sehemu nyingingi duniani.Tanzania pia ni nchi ambayo wanauzia magari yao,Beforward wanauza magari ya aina zote na kwa bei nafuu sana.
Jinsi ya kununua gari kupitia kampuni ya beforward.
i.Jisajiri kwenye website ya beforward(www.beforward.com),weka taarifa zako na majina yako kamili.
ii.Verify email(ingia kwenye gmail app ifungue email ya uthibitisho)
iii.Log in na uanze kutafuta gari unayoitaka.(fanya mawasiliano kwanza,hayo mawasiliano yawe ni yakiofisi.



.png)
Post a Comment