•Ni Rahisi kufanya miamala.
Katika swala la kutuma na kupokea ni rahisi sana, kwasababu mfumo wenyewe ndio ambao uthibitisha(blockchain technology),kama tulivyo kwisha kuangalia kwenye utangulizi ,ni hakuna mtu anayethibitisha miamala bali ni mfumo wenyewe ndio ambao uthibitisha miamala,kwaiyo ni kitendo cha haraka sana.
•Gharama ya kutuma ni nafuu.
Hapa tukiangalia ada ya kutuma hizi cryptocurriencies huwa inakuaga ni ndogo sana.Mfano Unaweza kutuma Litecoin hata za gharama ya 2000$ kwa ada ya 0.05$,Hivyo basi cryptocurriencies upunguza gharama za makato zaidi,bila shaka ni kwasababu ya kutokua na uhitaji wa watu katika swala zima la kufanya miamala.
•Hutumika na mtu yeyoye.
Hakuna vigezo vya mtu kuweza kuhusika kwenye soko la cryptocurrencies,Yani mtu yeyote anaweza kuhusika katika matumizi ya hizi fedha za kidigitali,Bila shaka kutokana na urahisi wake wa kununua upelekea mtu yeyote kuweza kumili fedha hizi za kidigitali.
•Huduma yake upatikana kwa masaa 24.
Ni muda wowote ule uweza kufanya miamala hata saa nane za usiku,Kama tulivyokwisha kujadiri hapo mwanzo,Kuwepo kwa mfumo huu wa blockchain na uwepo wa wasimamizi wachache hivyo upelekea system kuweza kufanya kazi masaa 24,Hapa inamaana mfumo huu utaliwa na computer software zaidi.
•Zina faida nzuri endapo ukiwekeza kwenye hizo fedha.
Hapa tukiangalia swala la uwekezaji katika fedha hizi za kidigitali mara zote uwa na faida nzuri,kama cryptocuriency uliyoichagua ikiongezeka thamani hivyo nawe utapata faida kama uliwekeza kwenye iyo fedha .Kama soko likienda vizuri uweza kupata faidi ata ya zaidi ya asilimia 100% ya kile ulichowekeza.
•Usalama ni mkubwa wakati wakufanya miamala.
Kutokana na kutokuwepo kwa mtu wakati kumepelekea usiri wa kufanya miamala,Hivyo katika mchakato mzima wa kutuma na kupokea digital currency utawaliwa na system ya blockchain uleta uaminifu mkubwa.
•Miamala inafanywa na mtumiaji yeye mwenyewe moja kwa moja.
Hii haitaji kwenda bank au kwa wakala,miamala yote unaweza kuifanya wewe kama wewe tena ukiwa umekaa na kifaa chako nyumbani mwako,Kwaiyo mtumiaji yeye kama yeye anaweza kufanya michakato yote ya ku trade (p2p,swap nk) hata akiwa nyumbani kwake.
•Baadhi ya fedha za kidigitali zimejikita kwenye sehemu moja.Mfano Ripple inatumika zaidi kwenye mambo ya malipo ya game.
Hii inaleta maana zaidi na urahisi wa kutumia ,mfano kama digital currency moja ikiwa inatumika kufanya malipo ya kitu fulani online ,hivyo huleta urahisi huduma na uhokoa muda kwani mchakato unakua ni waharaka sana.
•Ni rahisi sana kutuma kwenda nchi za nje.
Unaweza kutuma digital coin kutoka nchi moja kwenda nyingine tena kwa haraka zaidi na gharama nafu.Mchakato huu ufanya kwa dakika chache sana na kwa gharama nafuu,Kwaiyo hii ni njia nzuri sana kwa wafanyabiashara.
HASARA ZA FEDHA ZA KIDIGITARI
Kila kitu kizuri hakiwezi kukosa mapungufu,mapungufu yaliyopo kwenye mfumo huu ni machache tu:-Eb tuyaangalie haya,
•Hubadirika thamani kwa haraka zaidi.
Hizi fedha za kidigitali ubadirika thamani kwa haraka sana,hazina thamani maalumu inamaana leo inaweza ikawa na thamani kubwa ila kesho inaweza kupungua thamani au kupanda zaidi.Mfano ni kama bei ya mafuta ,hubadilika kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea duniani.Ila kwa kipindi hicho ambacho inabadilika kwa kupanda na kushuka unaweza kununua ama kuuza nabado ukatengeneza faida.
•Inaitaji uwekezaji wa muda murefu.
Hapa tunaangalia swala la faida nzuri,ili uweze kupata faida nzuri inatakiwa uwe mvumilivu sana. kwani kama ukiwa na haraka hutoweza kutengeneza faida nzuri.Faida utaipata Kama ukiiacha digital coin yako kwa muda murefu(ina maana unakua unasubiri ipande thamani)
•Inachukua muda mwingi kujifunza.
Hapa katika swala la Elimu hii ya fedha ya kidigital inaitaji muda zaidi kujifunza,kwaiyo lazima utumie muda mwingi ili uweze kuelewa vitu.kwasababu hakuna chuo wanachofundisha elimu hii,hivyo itakuitaji wewe kama wew uweze kutafuta maarifa haya sehemu mbali mbali.
Post a Comment