UTANGULIZI
Ni muhimu kuanza kumiliki fedha yako ya kidigitali,kwani hizi fedha ni asset(ni kitu ambacho upanda thamani kutokana na muda).
Ebu tuangalie mambo yanayoitajika ili uweze kumiliki hizi digital currency.yafuatayo ni mambo yanayoitajika ili uweze kumiliki cryptocurrency:-
i.Wallet ya kidigitali/Digital wallet.
ii.Pesa taslimu kwenye simu.
iii. aina ya cryptocurrency /fedha ya kidigitali unayoitaka.
iv.Gharama ya cryptocurrency.
v.Utafiti wa soko.
Ebu tuangalie jambo moja baada ya jingingine kati ya hayo hapo juu:-
i.Wallet ya Kidigitali/Digital wallet.
Wallet hutumika kuhifadhia,kutumia na kupokelea cryptocurrency,kama tulivyokwisha kujadiri kua hizi fedha za kidigitali huwezi kuzishika,hivyo ili uweze kuimiliki inatakiwa uwe na wallet yake ya kuhifadhia ,kutuma na kupokelea.Hizi wallet zinausalama mkubwa sana,lakini pia hizi wallet hutumika kufanyia biashara ya cryptocurrency na pia unaweza kujifunza zaidi hizi wallet,kwasababu ndani yake kuna makala mbalimbali na matukio mbali yanayohusu hizi cryptocurrencies.Mfano wa digital wallet ni binance wallet,Remitano wallet,coinbase wallet,Trust wallet,Tron link pro wallet ,nk.
ii.pesa taslimu kwenye simu.
Manunuzi ya hizi fedha za kidigitali yanafanyika mtandaoni ,kwaiyo inaitajika kua na pesa taslimu kwenye simu au bank.inatakiwa uwe na pesa kwenye mpesa,tigo pesa,airtelmoney,halopesa,au t-pesa,au hata kwenye accaunt yako ya bank.
Hapa uwepo wa pesa taslimu kwenye simu itakuwezesha kuweza kununua cryptocurrency yako online.Tunanunua hizi cryptocurrency online kwa njia ambayo inaitwa P2P trade,Hii ni njia maarufu sana yakununua hizi fedha za kidigitali mtandaoni.P2P trade hii njia rahisi sana na yakuaminika sana kwasababu huusisha manunuzzi ya hizi fedha baina ya watu wa jamii moja na kwa kutumia fedha za kawaida ambazo hutumika kwenye jamii hiyo,Mfano unaweza kununua kupitia :-Tanzania shilling(Tsh),kenya shillingi(Ksh).
iii.Aina ya cryptocurrency/fedha ya kidigital.
Hapa tunaangalia ni aina ipi ya fedha ya kidigitali ambayo unaitaka kwa lengo gani,Hizi fedha za kidigitali zimegawanyika katika sehemu kuu mbili,nazo ni cryptocurrency ambazo hazibadiliki thamani(stable coin)mfano,usdt,busd na cryptocurrency ambazo hubadilika thamani(unstable coin),mfano bitcoin,etherium,litecoin,ripple,Ada,Monero,nk.
iv.Gharama ya cryptocurrency.
Ni vyema ukajua bei ya cryptocurrency yako kwanza kabla ya kwenda kununua,Hizi fedha za kidigitali zinatofautiana bei.Kwa mfano bitcoin moja inauzwa kwa dollar 20000$ (Million 40 na kidogo),Etherium moja inauzwa dollar 1600$(Million 3na kidogo),usdt moja inauzwa dollar 1$ (2300Tsh).
Hivyo inatakiwa ujue gharama kwanza ili ujue kama utaweza kumudu kununua moja au utanunua kidogo.
v.Utafiti wa soko.
Unashauriwa kufanya utafiti wako binafsi kabla ya kununua cryptocurrency,kwasababu itakurahisishia kujua ni aina ipi au cryptocurrency gani ununue kwa wakati huo.Hapa tunaangalia vipengele viwili ,navyo ni fundamental analysis na techinical analysis.
Fundamental analysis:-Hapa tunaisoma asili ya hiyo cryptocurrency pamoja na habari zake kupitia mitandao ya kijamii,mmiliki wake na watu maarufu wanaojihusisha na biashara iyo.
Techinical analysis:-Hiki kipengele huusisha uchambuzi wa soko zima kwa kutumia graph na vichanganuzi mbalimbali kupitia App maalumu.

Post a Comment